Miongoni mwa masomo yanayojumuishwa kwenye mitihani hiyo ni Fiqhi, Aqida, Qur’an, Akhlaq, Historia ya Uislamu, na Saikolojia ya Kiislamu, ambapo walimu husika wameandaa maswali kwa umakini ili kuhakikisha kwamba wanafunzi wanapata nafasi ya kuonyesha maarifa na ustadi wao katika nyanja hizo.

10 Novemba 2025 - 13:55

Hawza ya Hazrat Zainab (sa) Yapima Ufanisi wa Kielimu Kupitia Mitihani ya Mwaka 2025 +Picha

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt as -ABNA- Wanafunzi wa Hawza ya Mabinti ya Hazrat Zainab (sa) iliyoko Kigamboni, jijini Dar es Salaam, wameendelea na mitihani yao ya muhula wa pili kwa mwaka wa masomo 2025. Mitihani hii ni sehemu ya tathmini ya kitaaluma inayolenga kupima uelewa wa wanafunzi katika masomo mbalimbali ya kidini na kielimu yanayofundishwa katika chuo hicho.

Miongoni mwa masomo yanayojumuishwa kwenye mitihani hiyo ni Fiqhi, Aqida, Qur’an, Akhlaq, Historia ya Uislamu, na Saikolojia ya Kiislamu, ambapo walimu husika wameandaa maswali kwa umakini ili kuhakikisha kwamba wanafunzi wanapata nafasi ya kuonyesha maarifa na ustadi wao katika nyanja hizo.

Hawza ya Hazrat Zainab (sa) Yapima Ufanisi wa Kielimu Kupitia Mitihani ya Mwaka 2025 +Picha

Uongozi wa chuo umeeleza kuwa maandalizi ya mitihani yalifanywa kwa umakini mkubwa, huku msisitizo ukiwekwa katika nidhamu, uadilifu, na mazingira ya utulivu kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi kufanya vizuri. Aidha, mitihani hii ni sehemu ya hatua muhimu kabla ya kuingia katika muhula mpya wa masomo unaotarajiwa kuanza mapema mwaka 2026.

Chuo cha Hawza ya Hazrat Zainab (sa) ni taasisi ya elimu ya kidini inayolenga kuwaandaa mabinti katika elimu ya Kiislamu kwa misingi ya maarifa, maadili, na huduma kwa jamii. Kupitia mfumo wa masomo unaochanganya elimu ya dini na sayansi za kijamii, wanafunzi hupata fursa ya kukuza uelewa mpana wa maisha ya Kiislamu ya vitendo.

Hawza ya Hazrat Zainab (sa) Yapima Ufanisi wa Kielimu Kupitia Mitihani ya Mwaka 2025 +Picha

Your Comment

You are replying to: .
captcha